Tunabadilisha maisha kupitia teknolojia na usalama wa kisasa
DJ Smartlink IT Solutions ni kampuni ya kitaalamu iliyoanzishwa mwaka 2025 na ipo Gezaulole, Kigamboni, karibu na stendi ya daladala, Wilaya ya Kigamboni, Dar es Salaam.
Tunajishughulisha na ufungaji na utoaji wa suluhisho za kisasa za Teknolojia na Usalama kwa nyumba, ofisi na biashara mbalimbali. Kuanzia ufungaji wa CCTV Cameras, mitandao (Networking), uzi wa umeme (Electric Fence), Gate Motors, Intruder & Fire Alarm Systems, hadi maendeleo ya tovuti na programu.
Tumejitolea kuwapa wateja wetu amani ya akili kupitia mifumo ya hali ya juu, ya kuaminika na rahisi kutumia. Tunaamini kuwa usalama na teknolojia ni haki ya kila mtu, hivyo tunatoa huduma bora kwa bei nafuu na ya kuaminika.
Tunatoa huduma na bidhaa za kiwango cha kimataifa.
Tunajenga mahusiano ya muda mrefu kupitia uaminifu na uwazi.
Tunaenda na teknolojia mpya ili kuwapa wateja wetu suluhisho bora zaidi.
Wateja wetu ni kipaumbele chetu cha kwanza.